Skip to main content
King County logo

Iliwekwa/ilisasishwa tarehe 16 Novemba, 2020:

Katika Kaunti ya King, Kesi au idadi ya maambukizi ya COVID-19 zimepanda juu sana kwa njia ambayo ni hatari sana na wagonjwa wanaolazwa hospitalini wamekua wengi sana. Tuna wasiwasi sana kuhusu kuongezeka kwa athari ya COVID-19 kwa afya ya jamii yetu, mfumo wa huduma ya afya, na uchumi. Novemba tarehe 15, Gavana Inslee alitangaza vikwazo vya muda mfupi vitakavyotumika katika jimbo lote hadi Disemba tarehe 14.

Vikwazo vipya ni kama vile:

 • Kukusanyika ndani ya nyumba na watu ambao hamuishi nao nyumba moja imepigwa marufuku/imekatazwa, isipokuwa kama ulikuwa karantini awali kwa siku 14 au ulikua karantini kwa siku 7 na ukapimwa na matokeo yako yakaonyesha huna virusi vya COVID-19.
 • Mikusanyiko ya nje isiwe na watu zaidi ya 5 ambao hamuishi nao nyumba moja.
 • Mikahawa na baa zitafungwa na hazitahudumia watu wakiwa ndani, lakini wanaweza kuendelea kutoa huduma kwa wale watakaobeba bila kukaa ndani na pia wanaweza toa huduma ya vyakula watu wakiwa nje kwa njia ya uangalifu sana.
 • Katika maduka ya rejareja, maduka ya vyakula na huduma za kibinafsi (kama vile., saluni za nywele na makucha, vinyozi, na kadhalika.) watu wanaoingia ndani wasizidi asilimia 25% .
 • Watu wanaoshiriki ibada za kidini ndani ya majengo wasizidi asilimia 25% au wasizidi watu 200, yoyote ile ambayo itakuwa na watu wachache. Kuimba kwa kikundi au kwaya hakuruhusiwi, lakini mwimbaji mmoja anaweza imba. Kuvalia maski au kufunika uso kunahitajika kila wakati.
 • Kila mtu anahimizwa kukaa nyumbani au katika mkoa wake na kuepuka safari ambazo si za lazima katika majimbo mengine au nchi zingine.

Tunajua ni nini inapunguza maambukizi na tunahitaji kufanya kile ambacho tunajua kitasaidia kupunguza maambukizi sasa:

 • Valia maski ukiwa karibu na watu ambao hamuishi nao katika nyumba moja (hata marafiki wa karibu na familia).
 • Kaa nyumba kadri inavyowezekana.
 • Punguza idadi, saizi na mara ambazo unahudhuria mikusanyiko—hasa ndani—na uongeze namna ya hewa safi kuingia ndani ya nyumba.
 • Nenda upimwe ukiona dalili yoyote ya ugonjwa au kama umekuwa karibu na mtu mwenye virusi vya COVID-19.
 • Njia salama zaidi ni kuepuka mikusanyiko na watu wanaotoka nje ya nyumba yako wakati huu wa msimu wa likizo.

VITU/SHUGHULI ZINAZORUHUSIWA
Novemba tarehe 17-Januari 11, 2021

Mbali na shughuli muhimu,mambo yafuatayo yanakubaliwa

Iliwekwa/ilisasishwa tarehe 15 Novemba

BURUDANI

 • Michezo kwa vijana na watu wazima (ifanyike nje tu,maski/barakoa inahitajika)
 • Uwindaji na uvuvi
 • Kuteleza juu ya theluji
 • Kwenda kambi
 • Golfu na tenisi
 • Burudani ya nje inayohusisha watu 5 au chini ya watu 5 wanaotoka nje ya nyumba yako
 • Mbio: kuendesha baiskeli,kukimbia,kuteleza juu ya theluji, na kufyatua risasi,mbio za mtumbwi na kayak,shindano la kukimbia,kuogelea na kuendesha baiskeli na mashindano mengine mengi ya michezo
 • Huduma za burudani majini (kwa wale tu watakaofanya miadi)

MIKUSANYIKO

 • Kukusanyika ndani ya nyumba na watu ambao hamuishi nao nyumba moja imepigwa marufuku/imekatazwa, isipokuwa kama ulikuwa karantini awali kwa siku 14 au ulikua karantini kwa siku 7 na ukapimwa na matokeo yako yakaonyesha huna virusi vya COVID-19.
 • Mikusanyiko ya nje isiwe na watu zaidi ya 5 ambao hamuishi nao nyumba moja.
 • Ibada za kidini ndani ya majengo watu wasizidi asilimia 25% au wasizidi watu 200, yoyote ile ambayo itakuwa na watu wachache. Maski inahitajika.(kwaya,bendi na mikusanyiko ya waimbaji hairuhusiwi,kuimba kwa kikundi hakuruhusiwi).
 • Huduma za kiimani za nyumbani au ushauri isizidi watu 5
 • Sherehe za harusi na mazishi au matanga watu wasizidi 30 (mikusanyiko ya maankuli hairusiwi)
 • Katika kituo cha kutoa huduma cha muda mrefu shughuli za kutembelewa zifanyike nje.(kutembelewa ndani ya kituo kiwe tu kwa watu wanaotoa msaada muhimu na hali za utunzaji wa huruma
 • Kusoma na watoto kusoma wakiwa nyumbani/kupitia kwa mtandao kunaruhusiwa kulingana na maagizo. ya idara ya elimu

KUSAFIRI

 • Kila mtu anahimizwa kukaa nyumbani au katika mkoa wake na kuepuka safari ambazo si za lazima katika majimbo mengine au nchi zingine.
 • Watu wanaofika kutoka majimbo mengine au nchi,ikiwa ni pamoja na wakaazi wa Washington wanaorudi,lazima wajiweke karantini kwa siku 14 baada ya kufika.

BIASHARA NA HUDUMA

 • Maonyesho ya wanyama wa majini (Akuariam) na bustani la wanyama (Maonyesho yawe nje tu)
 • Ujenzi
 • Mashamba
 • Nyumbani/huduma za nyumbani (mayaya/walezi,kusafisha nyumba, na kadhalika)
 • Maktaba (idadi ya wanaoingia ndani ipimwe/ikadiriwe)
 • Utengenezaji wa bidhaa
 • Maeneo ya kuonyeshea sinema bila kutoka garini
 • Makavazi/jumba la makumbusho (maonyesho yawe ya nje tu)
 • Huduma za kibinafsi (kama vile., saluni za nywele na makucha, vinyozi,tattoo na kadhalika.idadi ya wanaoingia ndani ipimwe kulinga na mahali wanapohudumiwa)
 • Utunzaji wa mnyama unayempenda
 • Huduma za kitaaluma/biashara zinazohusu ofisi (kufanyia kazi nyumbani kunahitajika kama inawezekana, biashara zina kiwango cha wanaoruhusiwa na haiwezi kufunguliwa kwa umma)
 • Biashara ya majengo(majumba yaliyowazi yamepigwa marufuku/kukatazwa)
 • Mikahawa/baa(kulia nje na kuondoka)
 • Maduka ya kuuzia(kununua ndani ya duka kunakubalika lakini idadi ya wanaoingia ndani iangaliwe wasiwe wengi/ikadiriwe)